Huyu ndiye hayati Oscar Kambona, mtangazaji aliyerusha matangazo ya kwanza ya Idhaa ya Kiswahili ya BBC tarehe 27 mwezi Juni mwaka 1957. Alifariki Uingereza akiwa na umri wa miaka 68. (Hii ni kwa manufaa ya wasomaji tu huyu Oscar Kambona ndiye alikua Bestman katika harusi ya Mwalimu Nyerere)
Abdulaziz Yacoub wa Idhaa ya Kiswahili akistajabia gari aina ya Rolls Royce muundo wa Silver Cloud kwenye maonyesho ya magari jijini London mwaka 1958.
Zeyana Seif mmoja wa watangazaji wa kwanza wa kike akiwa na wenzake mwaka 1959.
Mtangazaji Hassan Mazoa wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC akijiandaa kwa kipindi cha muziki enzi hizo.
Mtangazaji Alois Ngosso wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC akituma ripoti kutoka kwenye maonyesho ya kimataifa ya mashua kwa kipindi cha kila Jumamosi.
David Wakati mmoja wa watangazaji wa kwanza ambaye baadaye alirejea nyumbani Tanzania na kuwa mkuu wa redio ya taifa- RTD. (Hii ni kwa manufaa ya wasomaji, sasa hivi RTD imebadilishwa jina na kuitwa TBC-Taifa)
Watangazaji Athmani Magoma, Mohamed Salim Said Kwegyir Munthali na Hamza Kassongo wakiwa na Engela akiwaonyesha jinsi ya kutumia kinanda. (Hii ni kwa manufaa ya wasomaji Hamza Kassongo yeye bado anaendesha kipindi katika kituo cha Television cha Channel Ten, Dar es salaam)
Hao ndio waanzilishi wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC ambayo kwa sasa inafanya vizuri katika nchi hizi za maziwa makuu. Baada ya hao wakongwe, walifatia wengine kama akina Dustan Tido Mhando ambaye amefanya vizuri katika kituo hicho cha BBC, baada ya Tido Mhando kustaafu na kurudi Tanzania aliteuliwa kuwa kiongozi wa TBC(Tanzania Broadcasting Corporation). Na sasa kiongozi wa BBC idhaa ya Kiswahili ni ndugu Solomon Mugera.
Hao ndio waanzilishi wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC ambayo kwa sasa inafanya vizuri katika nchi hizi za maziwa makuu. Baada ya hao wakongwe, walifatia wengine kama akina Dustan Tido Mhando ambaye amefanya vizuri katika kituo hicho cha BBC, baada ya Tido Mhando kustaafu na kurudi Tanzania aliteuliwa kuwa kiongozi wa TBC(Tanzania Broadcasting Corporation). Na sasa kiongozi wa BBC idhaa ya Kiswahili ni ndugu Solomon Mugera.
2 comments:
Josh,
Thank you for taking us down the memory lane of the BBC Idhaa ya Kiswahili. It meant so much to me and my siblings since we have been searching to know just a little bit of our father, Kwegyir Munthali. When he was killed in a car accident we were 3, 2, 1 and my mother was expecting my brother who was born a month after my father's accident. Though we never got to know him, we have heard a lot of good things about him and we thank you for posting his picture (though with others) on this issue. He will be gone 44 years June 20th! It is good to know that some never forgot! Thank you so much! I am the eldest child of Kwegyir, living in America with my family and I was able to share this with my husband and my children, thank you so much!
Hapana, ngoja nikusahihishe kidogo.
Nyerere ndiye aliyekuwa Best Man wa Kambona kwenye harusi yake iliyofanyika hapo London. Nyerere alioa mwaka 1953 kabla hajaanza siasa na wala alikuwa hajafahamiana na Kambona wakati huo; alifungia harusi yake huko Musoma katika kanisa katoliki la Nyegina akisimamiwa na Padri William Collins. Wakati huo Kambona alikuwa bado ni mwanafunzi wa Tabora Boys, ambapo Nyerere alikuwa mwalimu wa St. Marys. Kambona alifunga ndoa na Flora mwaka 1960 katika kanisa la Mtakatifu Paul's Cathedral huko London wakiwa waafrika wa kwanza kufunga ndoa katika kanisa hilo; Julius Nyerere ndiye aliyekuwa Bestman katika hauris yao.
Post a Comment